ABU UBAYDAH
KHUTBAH 1
إِنَّ الْحَمْدَ لِلَّهِ، نَحْمَدُهُ وَنَسْتَعِينُهُ وَنَسْتَغْفِرُهُ، وَنَعُوذُ بِاللَّهِ مِنْ شُرُورِ أَنْفُسِنَا وَمِنْ سَيِّئَاتِ أَعْمَالِنَا.
مَنْ يَهْدِهِ اللَّهُ فَلَا مُضِلَّ لَهُ، وَمَنْ يُضْلِلْ فَلَا هَادِيَ لَهُ.
وَأَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ، وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ، وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا، وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً، وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ، إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا، يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ، وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا.
أُوصِيكُمْ عِبَادَ اللَّهِ وَنَفْسِيَ الْمُقَصِّرَةَ بِتَقْوَى اللَّهِ، فَاتَّقُوا اللَّهَ وَارْقُبُوهُ فِي السِّرِّ وَالْعَلَنِيَّةِ، وَاعْلَمُوا أَنَّ أَصْدَقَ الْحَدِيثِ كِتَابُ اللَّهِ، وَخَيْرَ الْهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَشَرَّ الْأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ، وَكُلَّ ضَلَالَةٍ فِي النَّارِ.
أَمَّا بَعْدُ...
Ayuhal haadhirun ....
Tukiwa katika siku hii tukufu ya wiki aliyoichagua Allah katika mwezi miongoni mwa miezi mitukufu aliyoijaalia Allah pale alipoumba mbingu na ardhi ... Ndugu zangu katika Imaan Barakallahu fykum
Bado tunaendelea na mada yetu kuhusiana na Nyumba za Allah, nyumba tukufu ambazo ni misikiti.
Nyumba ambazo Allah Ameamrisha zinyanyuliwe na zitukuzwe na pamoja na humo kutajwa jina lake na kusomwa Kitabu chake. Hii ni kama alivyosema Allah subhaanahu Wa ta'ala katika Aya tuliyotaja katika khutbah yetu ya ijumaa iliyopita
فِي بُيُوتٍ أَذِنَ ٱللَّهُ أَن تُرۡفَعَ وَيُذۡكَرَ فِيهَا ٱسۡمُهُۥ يُسَبِّحُ لَهُۥ فِيهَا بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ ٣٦
Katika nyumba ambazo Allah Ameamrisha zitukuzwe na humo litajwe jina lake. Wanamtakasa humo asubuhi [asubuhi na mapema] na [jioni mwisho wa mchana]
Tukawa ndugu katika Imaan tunataja na kutolea dalili makatazo ama mambo yasifaa kufanya katika nyumba za Allah.
Na kama tulivyosema kuwa jambo zima la aadab katika nyumba za Allah ni Jambo linalodhibitika katika Kitabu na Assunah na ya kwamba Maulamaa Allah awarahamu waliotangulia mbele za haki na awahifadhi waliohai wameifanya kazi suala hili Kwa kulitungia vitabu pamoja na kufanya duruus na kutoa fatawa mbalimbali juu ya suala hili ambalo tunahitajia kulijua ; Mimi pamoja na nyinyi na waislamu wote.
Hii ni kwa sababu misikiti inatuhusu na hivyo tunahitajia Ilm ya yanayohusiana na aadab zake. Hii ni Kwa mapana kuanzia tunayotakikana kuyafanya na tunayotakikana kuyawacha na inaanzia mbali kuanzia mtu anapokuwa nyumbani kwake akitaka kuja msikitini na anapokuja pamoja na kuingia na kuwa ndani yake na kuondoka kwake.
Mada hii ni pana ndugu katika Imaan ila sisi tumechagua - Kwa uwezo wa Allah - kuzungumzia na kukumbushana juu ya yale tunayopaswa kujiepusha nayo.
Katika khutbah ya ijumaa iliyopita tulitahadharisha juu ya mambo machache ikiwemo suala la Shirki na Bid'ah
Na alivyosema Allah subhaanahu Wa ta'ala
وَأَنَّ ٱلۡمَسَٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدۡعُواْ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدٗا ١٨
Na hakika misikiti ni ya Allah, basi msimuabudu yeyote pamoja na Allah
Hivyo tukasema enyi waja wa Allah kuwa msikitini haabudiwi yeyote isipokuwa Allah na pia ibaada ni zile ambazo ziko Katika Sheria ya Allah Kwa namna alivyotekeleza na kutuelekeza Mtume wake (ﷺ).
Msikitini au popote ibaada lazima iambatane na Sheria katika namna zake zote na kutakasiwa Allah.
Na ikiwa hii misikiti ni ya Allah na sio ya yeyote awe atakayekuwa - awe Imaam, mwenyekiti au yeyote yule atakayekuwa.!
Huenda hao wakawa ni wasimamizi tu - leo ni wao - Kesho ni wengine katika kusimamia na kuendesha na wala sio milki yao - hawawezi kuiweka katika mali yao wakairithisha.
Hivyo basi humu ibaada ni Kwa misingi ya Sheria pekee yake.
Yeyote asiwalazimishe au kuelekeza watu katika ushirikina sampuli yoyote - k.v kuwaomba wafu n.k wala Bid'ah za sampuli yoyote.
Humu ni Kwa Allah sio Kwa yeyote na anatiiwa Allah na wala sio yeyote
عَنْ عَلِيٍّ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ‏.‏
Kutoka Kwa Ali (Allah amridhie) kutoka Kwa Mtume (ﷺ)
Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Allah Aliyetukuka na kutakasika.
Tukataja makatazo ya kutangaza vilivyopotea msikitini na matangazo yasiyo kichwa wala mguu na makatazo na kufanya biashara - kuuza au kununua na zinaingia pia biashara za simu zama hizi.
Kwa hakika misikiti haikujengwa Kwa ajili ya haya Kwa ajili ya ibaada.
Tukataja juu ya kuwaudhi waislamu wengine kwa kunyanyua sauti katika usomaji na katika Swala huku kila mtu anaswali kivyake Kwa sauti.
Inaingia humu kelele zisizo na msingi katika kupiga gumzo na kuimbaimba katika vilivyozuliwa na vya haraam na kusikiza miziki n.k katika simu zetu. - asiyekuwa na simu angelijua angelimshukuru Allah. Zimeharibu mengi.!
Leo katika nyumba za Allah watu ni kuzungumza tu yasiyofaa na kupiga porojo za dunia.
Si siasa, si ushabiki wa timu zao. Yaani imekuwa dunia na Sisi, Sisi na dunia... Wallahu Musta'an
وَعَنِ الْحَسَنِ مُرْسَلًا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَأْتِي عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ يَكُونُ حَدِيثُهُمْ فِي مَسَاجِدِهِمْ فِي أَمْرِ دُنْيَاهُمْ. فَلَا تُجَالِسُوهُمْ فَلَيْسَ لِلَّهِ فِيهِمْ حَاجَةٌ» . رَوَاهُ الْبَيْهَقِيّ فِي شعب الْإِيمَان
"Zitakuja katika watu zama ambazo itakuwa katika mazungumzo yao katika misikiti Yao ni katika mambo ya dunia yao. Usikae pamoja nao Kwa hakuna kwa Allah kwao haja yoyote"
سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ يَقُولُ: «مَنْ جَلَسَ فِي الْمَسْجِدِ» ـ أَوْ «مَنْ جَلَسَ فِي الْمَجْلِسِ» ـ «فَإِنَّمَا يُجَالِسُ رَبَّهُ، فَمَا أَحَقَّهُ أَنْ لَا يَقُولَ إِلَّا خَيْرًا».
Sa’iyd bin Musayyib amesema:
“Pindi mtu anapokaa Msikitini, kwa hakika anakaa kwa ajili ya kumuabudu Rabb wake, kwa hiyo, aongee tu kwa lile ambalo ni jema.” [Tafsiyr Al-Qurtwubiy].
Idhan, ni kupita tu na kukumbushana pamoja na kutilia mkazo Kwa yale tuliyoyazungumzia ijumaa iliyopita katika suala zima la nyumba za Allah katika mambo yasiyofaa.
Leo bi Idhnillah Al Karim tutaendelea na mada hii na kutaja makatazo mengine kwa dalili insha'Allah...
Ndugu katika Imaan, katika hili la kutowaudhi watu msikitini pia tunatoa nasaha na kuwakumbusha wale ambao huenda na watoto katika nyumba za Allaah kuwa, wanawajibika kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha kuwa tabia zao (watoto) haziwasumbui watu wengine wanaofanya ‘ibaadah.
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
أَلاَ فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ‏
“Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja mmoja ataulizwa kuhusiana na wale walio chini ya uangalizi wake.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim]
Licha ya Hadiyth hii kuwa na maana ya ujumla, bila shaka, inatumika pia kwa wale ambao wanakwenda na watoto katika nyumba za Allaah.
Mzazi (Mlezi) anatakiwa kuwafundisha wale walio chini yake, tabia (taratibu) njema za kutembelea nyumba za ‘ibaadah.
Asimruhusu mtoto wake kukimbia kimbia ovyo Msikitini (hali itakayopelekea) kuwasumbua wengine wenye kujikurubisha kwa Allaah.
Kama mtoto ni mdogo sana na hawezi kuzielewa taratibu hizi (za kukaa Msikitini), basi ni bora kumuacha nyumbani kuliko kuwabughudhi wengine walioko Msikitni.
Katika kuepuka Jambo la kuwaudhi waislamu pia ni lazima kwa mtu anayetaka kwenda Msikitini kuhakikisha kuwa hana harufu mbaya.
Hii ni kutokana na kauli ya Allaah katika Qur-aan:
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ
“Enyi wana-Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid (mnapokwenda Misikitini kwa ajili ya ‘ibaadah)” [Al-A‘raaf: 31].
Pia, maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyopokelewa kutoka kwa Jaabir bin Abdullah katika Sahih Muslim [vile vile Kwa maimamu wengine wa hadith kwa riwayah nyinginezo kama Al Imaam Bukhari katika Sahih yake] :
مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ - فَلاَ يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا
"Yeyote aliyekula vitunguu maji, au vitunguu thaumu au liki (aina ya vitunguu) asihudhurie Msikitini kwetu." [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].
Ushahidi tulioutoa hapo juu unatudhihirishia kuwa ni wajibu kwa Muislamu kuhakikisha kuwa hatowaudhi watu wengine kutokana na harufu (mbaya) ya mwili (wake) anapohudhuria Msikitini, na kwa hiyo, anapaswa kujitahidi kadiri awezavyo kujisafisha kabla ya kuhudhuria Swalah katika nyumba ya Allaah.
Maulamaa wanasisitiza juu ya katazo hilo tulilolitaja na kwamba linaenea zaidi pia kwa uvutaji sigara, kutokana na harufu mbaya ya sigara anayobaki nayo mvuta sigara mara tu amalizapo kuvuta sigara.
Harufu hii (ya sigara), bila shaka, ina madhara na huwasumbua wanaoswali katika Msikiti, na pia huwasumbua (huwaumiza) Malaika.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
فَإِنَّ الْمَلاَئِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ ‏
“Kwa hakika Malaika huumia kwa kile ambacho huwaumiza bin Aadam.” [Swahiyh Muslim].
أَقُوْلُ مٓا تٓسْمٓعُون، وَأَسْتَغْفِرُ اللهَ
ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارٗا
KHUTBAH 2
الْحَمْدُ لِلَّهِ حَمْدًا كَثِيرًا طَيِّبًا مُبَارَكًا فِيهِ، كَمَا يُحِبُّ رَبُّنَا وَيَرْضَى.
وَأَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ.
اللَّهُمَّ صَلِّ وَسَلِّمْ وَبَارِكْ عَلَى نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ، وَعَلَى آلِهِ وَصَحْبِهِ أَجْمَعِينَ، وَمَنْ تَبِعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ.
ِّقَالَ أَبُو جُهَيْمٍ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم
لَوْ يَعْلَمُ الْمَارُّ بَيْنَ يَدَىِ الْمُصَلِّي مَاذَا عَلَيْهِ لَكَانَ أَنْ يَقِفَ أَرْبَعِينَ خَيْرًا لَهُ مِنْ أَنْ يَمُرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ
‏.‏ قَالَ أَبُو النَّضْرِ لاَ أَدْرِي قَالَ أَرْبَعِينَ يَوْمًا أَوْ شَهْرًا أَوْ سَنَةً
Anasema Abu Juhaym kuwa amesema Mtume (ﷺ)
“Lau mtu anayepita mbele ya mtu anayeswali angelijua uzito wa kosa lake hilo, ingelikuwa bora kwake kusubiri arobaini kabla ya kupita mbele ya mtu anayeswali.”
[Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].
Anasema Abu Nadhr (mmoja katika wapokezi wa hadith hii) kuwa sikumbuki kama alisema siku arubaini au miezi arubaini au miaka arubaini.
Katika hadithi hii tunaona katazo la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kupita mbele ya anayeswali.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ ‏- رضى الله عنه ‏- قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏- صلى الله عليه وسلم ‏-{ إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ إِلَى شَيْءٍ يَسْتُرُهُ مِنْ اَلنَّاسِ , فَأَرَادَ أَحَدٌ أَنْ يَجْتَازَ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلْيَدْفَعْهُ , فَإِنْ أَبَى فَلْيُقَاتِلْهُ , فَإِنَّمَا هُوَ شَيْطَانٌ } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ .‏"
“Mmoja wenu anaposwali kuelekea kitu kinachomzuia (kutoka kwa kupitwa mbele yake), halafu mtu akataka kupita mbele yake, basi na amzuie. Akiendelea kung’ang’ania, basi na apigane naye, kwa hakika huyo ni shetani.”
— Imepokewa na Bukhari na Muslim
"وَفِي رِوَايَةٍ : { فَإِنَّ مَعَهُ اَلْقَرِينَ } .‏"
Na katika riwaya nyingine:
"Kwa hakika yuko pamoja rafiki (shetani)."
Pia ndugu katika Imaan, ni juu ya Imaam au munfarid (anayeswali pekee yake) kuzingatia jambo la sutrah.
Ndugu katika Imaan, khutbah hii haitutoshi kubainisha na kuzungumzia suala zima mtu kuweka sutrah. Huenda lisitupelekee tu kutoka katika mada bali pia na katika kutoka katika muda mfupi tulionao katika khutbah yetu. Allah akitujaalia insha'Allah tutaweka mfulizo wa khutbah zake - tukijaaliwa uhai na afya na Allah tunamtaka msaada.
Hata hivyo maneno tuliyotaja ya Mtume (ﷺ) yametosha kuonyesha uharamu wa kupita mbele ya anayeswali na uwajibu wa kuweka kuweka Kwa Imaam au munfarid (anayeswali pekee yake) kama walivyoeleza baadhi ya maulamaa. Na hilo tunaliachia hapo hadi atapojaalia Allah subhaanahu Wa ta'ala.
عباد الله
Masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah yanakaribia kwa kasi — siku hizo zitaanza kabla hatujakutana tena Ijumaa ijayo.
Ndio maana kabla ya kushuka katika mimbari hii nimependa kugusia
Haya ni masiku yenye fadhila kubwa mno. Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema:
«ما مِن أيامٍ العَمَلُ الصَالِحُ فِيها أحَبُّ إلى الله مِن هَذِه الأيام»
Yaani: “Hakuna masiku ambayo matendo mema yanapendwa zaidi na Allah kuliko katika masiku haya.”
— [Bukhari].
Hivyo basi, tujipange mapema:
Tuimarishe ibada zetu,
Tujiandae kufunga, kufanya dhikr nyingi, kuswali zaidi, na kutoa sadaka,
Tujitahidi siku ya Arafah, tukifunga kwa thawabu zake.
Na In shaa Allah, khutbah maalum kuhusu masiku haya itakuja, lakini huu ni ukumbusho wa mapema ili tusikose maandalizi.
اللَّهُمَّ اجعلنا مِنَ الَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ الْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُ،
اَللَّهُمَّ اجْعَلْنَا مِمَّنْ يُعَظِّمُونَ بُيُوتَكَ، وَيَعْرِفُونَ حُرْمَتَهَا، وَيَقِفُونَ عِندَ آدَابِهَا، وَلَا يَجْعَلُونَهَا لِلَّهْوِ وَالضَّحِكِ وَالقِيلِ وَالقَالِ.
اَللَّهُمَّ طَهِّرْ مَسَاجِدَنَا مِنَ اللَّغْوِ وَاللَّعِبِ وَالْهَمْسِ وَالْكَثْرَةِ فِي الْكَلَامِ، وَاجْعَلْهَا دُيُورًا لِذِكْرِكَ، وَتِلَاوَةِ كِتَابِكَ، وَتَعْلِيمِ دِينِكَ.
اَللَّهُمَّ أَصْلِحْ أَحْوَالَنَا وَأَحْوَالَ أَئِمَّتِنَا، وَخُصَّ بِالدُّعَاءِ إِمَامَنَا مُحَمَّدٍ خَمِيس، اَللَّهُمَّ أَنْعِمْ عَلَيْهِ بِالصِّحَّةِ وَالْعَافِيَةِ، وَبَارِكْ فِي أَهْلِهِ وَذُرِّيَّتِهِ، وَثَبِّتْهُ عَلَى الْمَنْهَجِ الصَّحِيحِ، مَنْهَجِ السَّلَفِ الصَّالِحِ، مَعَ سَائِرِ أَئِمَّةِ الْهُدَى، وَاجْعَلْنَا مَعَهُمْ فِي سَبِيلِكَ الْمُسْتَقِيمِ.
اَللَّهُمَّ اشْفِ مَرْضَانَا وَمَرْضَى الْمُسْلِمِينَ، وَارْحَمْ مَوْتَانَا وَمَوْتَى الْمُسْلِمِينَ، وَارْزُقْنَا حُسْنَ الْخَاتِمَةِ، وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا.
وَصَلِّ اللهمَّ وَسَلِّمْ وَبَارِكْ عَلَى نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ، وَعَلَى آلِهِ وَصَحْبِهِ أَجْمَعِينَ، وَعَلَى مَنِ اتَّبَعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ.
عِبَادَ اللهِ،
إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَى، وَيَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ، يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ.
فَاذْكُرُوا اللَّهَ يَذْكُرْكُمْ، وَاشْكُرُوهُ عَلَى نِعَمِهِ يَزِدْكُمْ، وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ، وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ.
وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ
Published using